Michezo

Tumekuwa binadamu-Washangilia wanawake Saudi Arabia kwa kuingia uwanjani

Hatimaye wanawake nchini Saudi Arabia wameingia kwa mara ya kwanza kwenye viwanja vya mpira kushuhudia mchezo huo pendwa zaidi duniani.

Wanawake hao waliohudhuria kwenye mchezo wa Derby ya Ryadh kati ya Al-Nassir FC na Al-Hilal FC kwenye Uwanja wa Taifa wa King Fahad wikiendi iliyopita walionekana wenye furaha huku wengi wakiimba kuwa wamekombolewa na wamekuwa binadamu wa kawaida kama wanawake wengine duniani.

Wanawake hao ambao waliongozwa na mwanaharakati  Madeha al Ajroush (63) ambaye ndiye amekuwa akipigania haki za wanawake kuingia viwanjani na kuendesha magari tangu akiwa na miaka 18, amesema ni furaha kuona malengo yake yamekamilika ingawaje umri umemtupa mkono.

Tangu nikiwa na miaka 18 nilijua itafika muda wanawake tutaendesha magari na kuingia kwenye viwanja na kweli imetimia ingawaje hatua imechelewa hadi sasa nina miaka 63 lakini imenipa funzo katika maisha yangu,“amesema Bi. Al Ajroush ambaye amefungwa zaidi ya mara tatu akipigania usawa wa kijinsia nchini Saudi Arabia.

Wanawake wengine walioonekana uwanjani hapo walisikika wakiimba na kushangilia kwa furaha sio kwa sababu ya mpira bali kutokana na kuruhusiwa kuingia viwanjani.

Tunajiona kama tumekuwa binadamu kwa sasa kwani tunaweza kujiamulia kipi cha kufanya na sio kuamuliwa na mtu kama ilivyo kuwa awali,“amesikika Mwanafunzi wa kike wa miaka 18 kwenye mahojiano na Sky News.

Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya mwaka jana nchi hiyo kuruhusu wanawake kuendesha magari na kuanza kuingia viwanjani kuanzia mwaka huu.

Awali wanawake nchini humo walikuwa hawaruhusiwi kuingia viwanjani lakini kuanzia mwaka huu wataingia kwenye viwanja vya michezo kwa masharti ya kujifunga Hijab na Niqab.

Soma zaidi – Saudi Arabia kuruhusu wanawake kuendesha magari


Tangu aingie madarakani Mwana wa Mfalme wa nchi hiyo, Mohammed bin Salman (32) amekuwa akitoa ahadi za kuibadilisha Saudi Arabia kuwa nchi ya kisasa kwa kuboresha uchumi, miundo mbinu na masuala mbalimbali ya kijamii huku akikiri wazi kuwa jambo hilo litakuwa na changamoto ingawaje litakuwa la faida kwa kizazi kijacho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents