Habari

Tumieni mawasiliano ya simu kuboresha huduma za jamii – Prof. Mbarawa

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ameyataka makampuni ya simu nchini kuhakikisha mawasiliano ya simu yanatumika kuboresha huduma za jamii kama elimu.

Waziri Mbarawa ameyazungumza hayo wakati akikagua na kuzindua minara ya simu ya kampuni za VODACOM, TTCL,HALOTEL, na TIGO katika Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Profesa Mbarawa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na kampuni za simu kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF.

“Tumieni mawasiliano ya simu kufanya biashara, kuboresha huduma za jamii kama elimu na habari ili kukuza ustawi wa maisha yenu”, amesema Profesa Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa amewaonya wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya simu kwani ipo sheria kali inayodhibiti matumizi mabaya ya simu.

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Mhandisi Peter Ulanga amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa mfuko huo umejipanga kukamilisha miradi yote kwa wakati na kufanya uhakiki wa takwimu za mawasiliano nchi nzima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents