Burudani

Tumpigie Kura Mwisho!!

Mwisho na Paloma wa Zambia wamechaguliwa kupigiwa kura za kuobaki katika jengo hilo wiki hii, na ikiwa ni mara ya  kwanza kwa Mwisho kupendekezwa katika mtanange huo, huku Munya akiwa amependekezwa mara sita  mfululizo na kuokolewa. Tumpigie kura Mwisho kwa kutuma SMS ‘VOTE Mwisho‘ kwenda namba 15726 ama kwa kutembelea tovuti ya Big Brother Africa http://bigbrotherafrica.dstv.com/Vote/

Mwisho Mwaipamba anayeiwakilisha Tanzania katika shindano la BBA All Stars ameonekana kuwa kipenzi kwa watazamaji katika mchezo huo, na imewapelekea wengi kuanza kusema labada anaweza kujinyakulia kitita cha dola 200,000 katika fainali za mchezo huo.

 

Mwisho na Munya mara nyingi wamekuwa wakionyesha ubababe kila mmoja akimweleza mwenzake  kuwa pesa hizo aterejea nazo kwao.Hata hivyo Munya hakukubali alipaza sauti kwa nguvu akipanda ngazi na kumwabia Mwisho niachie pesa zangu, Mwisho ambaye alielekea bafuni akamwambia mimi ndio kinara katika mchezo huu.

Hata hivyo Merly ambaye ni mpenzi wake Mwisho alicheka na kuvunjika mbavu kwa mabishano yao.

Mwisho amekuwa aking’ara kulioko washiriki wenzake ndani ya jengo hilo na pia amekuwa amekuwaburudani ya tosha kutokana na yeye kupenda kunywa pombe na sigara  pamoja  na vituko vinavyosisismua na kumfanya kuoneka wa kipekee katika jumba hilo, huku Munya akionekana kama katuni kwenye jengo hilo.

Uti naye ameonkekana kuwa mpinzani wa Munya baada ya kumpiku kwa kura 2 akiwa amepata kura 8 huku Munya akipata kura sita na Code akiambualia kura moja kuota nchini kwake Malawi.

Kutokana na uchache wa kura alizopata Code ametolewa na kupelekwa zizini.
Nchi zilizompigia kura Uti ni Angola.Ethiopia, Ghana, Kenya, Msumbiji, NIgeria, Tanzania na Uganda. Huku Munya akiwa amepigiwa kura na nchi ya Botswana, Namibia, Afrika ya Kusini, Zambia, Zimbambe na nchi za Afrika.

Wiki iliyopita Mwisho alikuwa mkuu wa jumba hilo alimweleza Munya kuwa amekwisha kwani amempendekeza apigiwe kura kwa kuliokoa jina lake.
Munya akasema kuwa anakwenda kupaki nguo zake na kuondoka nyumbani, baadaye IK akamweleza kuwa BB Afrika wanamtaka aendelee kubaki, na washiriki wenzake wakacheka kusikia hivyo.

Baada ya Code kutoka amemwacha Jen peke yake ambaye alikuwa rafiki yake na kujikuta hana rafiki ndani ya jumba hilo.

Meryl alisema kuwa Jen amebaki mpweke na wanapaswa kumwingiza katika kundi hilo.

Uti na Mwisho waliunga mkono Meryl na kusema Jen sasa ni mmoja wao.Walisema kuwa Meryl atumie cheo chake cha ukuu wa jumba  hilo wiki hii kuhahikisha anamwokoa yeyote atakayeingia katika mtanange wa kupigiwa kura.

Baada ya Mwisho kuondoka katika Ukuu wa jumba hilo Uti na Merly walizungumzia nani wa kumpendekeza atoke,Meryl akasema Paloma sababu amevunja uaminifu  wake kwa Kaone. Hata hivyo Meryl alisema kuwa Mwisho alifanya Ujinga kumweka Munya na Uti sababu alimweka Uti kwenye hatari.

Na katika jumba la shamba Yacobo wa Ethiopia ameamua kurudi  nyumabni kwao hawezi kuvumilia maisha ya shamba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents