Habari

Tunadhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya watumishi – Waziri Mkuu

Waziriri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itadhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya watumishi wa umma na italipa madeni yote ya watumishi ambayo yamehakikiwa na kukutwa kuwa ni halali.

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwenye mkutano uliofanyika kata ya Goweko, wilayani Uyui mkoani Tabora.

“Hivi sasa tunadhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya watumishi, hakuna madeni ya matibabu, ya likizo au ya masomo. Kila mtumishi anaruhusiwa kujiendeleza, lakini ni lazima kwanza aandike barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuelezea nia yake na akikubaliwa, ndipo aanze kutuma maombi kwenye vyuo,” alisema Waziri Majaliwa.

“Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli alisitisha malipo sababu ya zoezi la kubaini watumishi hewa, sasa kazi hiyo imeshakamilika, yale yaliyobainika kuwa ni halali yatalipwa. Tunataka watumishi mfanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa bidii.”

Waziri Mkuu ameweka utaratibu wa kukutana na watumishi wa umma kila anapofanya ziara za kikazi mikoani, aliwaeleza watumishi wa wilaya hizo kwamba Serikali imeanzisha mfumo wa kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents