Michezo

Tunahitaji kucheza kama bingwa mtetezi – Tshishimbi

Mara baada ya kukamilika kwa duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara kiungo mkabaji raia wa DR Congo, Papy Kabamba Tshishimbi amekiri kuwa ligi ya Tanzania ni ngumu na yenye ushindani mkubwa hali inayolazimu kujiandaa muda wote kila baada ya kumalizika kwa mchezo.

Tshishimbi ambaye ametokea katika timu ya Mbambane Swallows ya Swaziland ameyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa klabu ya Young Africans.

“Ligi ya Tanzania ni ngumu na yenye ushindani mkubwa hupaswi kudharau timu unatakiwa kujiandaa vyema kwa kila dakika 90 unazokwenda kuzikabili,” amesema Tshishimbi.

Tshishimbi ameongeza kuwa “Sifikirii tena kuhusu sare ya mchezo uliopita, mimi na wachezaji wenzagu tumejindaa vizuri kwa ajili ya michezo ijayo,tunahitaji kucheza kama mabingwa ili kutetea ubingwa”.

Yanga SC ilicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Agosti 27,2017 dhidi ya Lipuli FC na kulazimishwa sare ya mabao 1-1.

Lipuli ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji, Seif Abdalah Karihe kunako dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza kisha,  Donald Ngoma kuisawazishia Yanga SC dakika 45 kabla ya mapumziko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents