Habari

Tunataka watu wanaofanya kazi kwa faida – Rais Magufuli (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe amemuagiza Msajili wa hazina kuhakikisha mashirika na Taasisi yenye kustahili kutoa gawio kwa serika zianze kutoa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Juni 21, 2018 wakati akipokea gawio la sh. Bilioni 1.5 kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), ambapo amesema kuwa anataka watu wanaofanyaka kazi kwa faida.

“Napenda kutumia fursa hii kuagiza Taaisisi na mashirika mengine yenye kustahili kutoa gawio kutoa gawio kwa serikali kufanya hivyo nafahamu kuwa tunataribani mashirika zipatazo 91 zenye kutoa gawio na zinazostahili kutoa gawio serikalini lakini si zaidi ya mashirika au Taasisi 50 ndiyo yamekuwa yakitoa gawio kwa serikali,” amesema Rais Magufuli.

“Namuagiza msajili wa hazina sijui kama yupo hapa, ahakikishe mashirika na Taasisi kulipa ambao watashindwa tumia sheria, kama nikufukuza fukuza, kama nikuyafuta futa tunataka watu wanaofanya kazi kwa faida.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents