Tunatumai Kilio Chetu Raisi Kenyatta Amekisikia, Nitakuja Uganda Kwa Media Tour! – Dogo Richie

Msanii Dogo Richie kutoka Kenya, amefunguka mengi kuhusu jinsi wasanii nchini Kenya wamekua wakipitia hali ngumu kupata kipato cha kila siku baada ya uchumi wa nchini humo kufungua kwa takrabani miezi saba iliyopita kwa sababu ya kuzuia kuenea kwa kasi kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona.

Akiongea na runinga ya Record ya nchini Uganda, Dogo Richie amesema wasinii wamelia sana maana wamekua wakitegemea matamasha mbali mbali ili kutoa burudani kwa mashabiki wao na malipo yake ni fedha ili waweze kujiendeleza kimaisha.

Lakini mambo yameenda kombo pindi tu marufuku yakutokusanyika kwenye kumbi za burudani na maeneo ya hadhara nchini humo kwa kuzuia Corona. Dogo Richie amesitiza kua, wasanii wenye uwezo wakurekodi muziki na wasanii A list kama yeye ndio wamekua na bahati ya kutoa nyimbo na kuzisambaza kwenye media tofauti. Huku wasanii chipukizi wakiwa hoi hawajui wapi pakuanzia wala kumaliza.

Lakini pia Dogo Richie ametoa mwangaza kua, huenda uchumi wa nchini Kenya ukafunguliwa wiki ijayo. Hii ni baada ya kuulizwa na mtangazaji wa Record TV, anapanga kuuzuru Uganda lini ili kuitangaza kazi yake mpya kwa jina Sina Habari Nao, ambayo alitoa ili kuangazia maswala ya ufisidi unao ikumba sekta ya muziki Kenya. Chini hapa ni video mpya ya Kazi hiyo ya Sina habari nao.

Na Changez Ndzai Kenya

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW