Habari

Tundu Lissu aahidi kuboresha Uchumi

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema Serikali yake itaboresha sekta zote za kiuchumi, kikiwamo kilimo, uvuvi na maslahi ya watumishi wa umma, iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Mgombea Urais huyo wa Chadema, Tundu Antipas Lissu, ameyasema hayo alipohutubia mkutano wake wa kampeni, uliofanyika Uwanja wa Mnada wa Ng’ombe, Mjini Bariadi, mkoani Simiyu.

“Tutajenga nchi ya watu huru, tutajenga nchi ya watu wenye haki tutajenga nchi yenye maendeleo ya watu, wavuvi wote ni kilio cha kuumizwa cha kuchomewa mitumbwi yao, wakulima wa pamba ni kilio , nimekuja hapa ndugu zangu bariadi kuwaomba mnipigie kura niwe rais wenu”  alisema Tundu Lissu

Katika hatua nyingine, Tundu Lissu, amebeza utaratibu uliotumika kuandaa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo machinga, huku akitaka pia Uchaguzi kuwa wa huru na haki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents