Habari

Tundu Lissu amaliza matibabu yake Ubelgiji, Ahofia kurudi Tanzania kisa ‘Watu wasiojulikana’ (+video)

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu amesema kuwa kwa sasa amemaliza matibabu yake nchini Ubelgiji ila bado anahofu ya kurudi Tanzania.

Akiongea kwenye mahojiano yake na idhaa ya kiswahili ya VoA, Lissu amesema kwa sasa hana kisingizio cha matibabu kwani amemaliza matibabu ila anashindwa kurudi Tanzania kwa kuhofia usalama wake.

Lissu amesema watu wasiojulikana waliomshambulia miaka miwili iliyopita bado hawajakamatwa, Hivyo anasubiri hadi apate uhakika wa usalama wake.

https://www.instagram.com/tv/B3bL2ObhfzG/?igshid=1p5xy5ulsafgd

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents