Michezo

Tunisia ya mtupia virago kocha wao Henryk Kasperczak

Kocha maarufu, Mpoland Henryk Kasperczak ameondolewa kuifundisha timu ya taifa ya Tunisia, inayowania kucheza fainali za kwanza za Kombe la Dunia tangu mwaka 2006, imeachana na Kasperczak tangu wikiendi iliyo pita.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 70, ambaye aliiongoza Tunisia kufika fainali ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 1996 kabla ya kuondoka nakarejea kazini mwaka 2015.

Tunisia ilifungwa na kutolewa katika robo fainali kwenye za kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon na vipigo vya kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Cameroon na Morocco vilichangia kutupiwa virago kwa kocha huyo.

Tunisia wanakabiliwa na mechi ya nyumbani na ugenini dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 kati ya Agosti na­ Septemba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents