AwardsBurudani

Tunzo Mpya za Kili

Hatimaye safari ya mchakato wa kuwapata washindi wa Tunzo za Muziki Tanzania umefikia ukingoni na msanii Sean Kingston kutoka Marekani ndiye atapamba hafla hiyo na kushiriki kwa kutoa Tunzo ya wimbo bora wa RAGGA.

Wakiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo hii katika ukimbi wa mikutano wa kampuni ya bia TBL, Mkurugenzi wa masoko wa TBL, David Minja (kati) akiwa na Mratibu wa BASATA, Angelo Luhala (kushoto) pamoja na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe kwa pamoja wameonyesha mfano wa tunzo watakazopewa wasanii washiriki wa Kili Music Awards.

Mchakato wa upigaji kura ulianza rasmi tarehe 1 mwezi Aprili 2010 na unaendelea hadi tarehe 13.Mei.2010. Taarifa kamili kuhusu mchakato huu unapatikana kupitia tovuti ya http://www.kilitimetz.com pamoja na vipeperushi na magazeti mbali mbali.

Tarehe 14 mwezi wa Mei ndio usiku wa kuwatunuku washindi katika vinyang’anyiro mbali mbali vya Tunzo za Muziki Tanzania. Usiku huu ni kwa mwaliko tu. Wana habari watapata mialiko kupitia vyombo vyao vya habari na kutakuwa na pasi maalumu kwa ajili yao ikiwa ni pamoja na eneo lao liliotengwa mahksusi kuwawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi.

Usiku huo utapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wa ki Tanzania pekee.
Nao ni:

1. AY.
2. Fid Q.
3. Joh Makini.
4. Marlow.
5. African Stars – Twanga Pepeta.
6. Mwansiti.
7. Lady Jaydee.
8. Mzee Yusuph na Offside Trick
9. Wahapahapa
10. Ali Kiba

Mwaka huu Kilimanjaro Premium imeboresha zawadi mashindano hayo pamoja na Tunzo yenyewe.
1. Zawadi za pesa taslim zitakazotolewa kwa ujumla ni TZS 15M.
2. Katika maboresho ya Tunzo zenyewe, Tunzo mbili kubwa za Hall of Fame zitakua “GOLD PLATED”.
3. Kila mteule na mshindi watapata cheti cha utambulisho wa ushiriki wake katika Tunzo za Muziki Tanzania.

Taarifa kamili na ujio wa msanii Sean Kingston zitatolewa katika mkutano na wana habari utakaofanyika tarehe 13. Mei. 2010.

Taarifa ya ziada

Kilimanjaro Tanzania Music Awards inayofuraha kuwakaribisha Malaria No More (MNM) katika kinyang’anyiro cha Msanii bora Anayechipukia.Malaria No More (MNM) wameongeza thamani Tunzo hiyo kwani mshindi atakayepatikana atakwenda nchini Senegal katika shughuli na onyesho la pamoja na Msanii mkongwe wa Africa anaefahamika kwa jina la Youssou N’dour.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents