Burudani

Tuokoe maisha muda wa kuokoa hip hop ulishapita – Madee

Msanii mkongwe wa muziki, Madee Ali amedai kitendo cha yeye kubadilika kutoka kwenye hip hop ngumu na kuamua kuimba na kupata mafanikio kwenye muziki huo kimewafanya wasanii wengi wagumu kuiga nyayo zake.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Madee amedai Darassa na Roma ni kati ya wasanii ambao wamebadilika na kuona mafanikio ya mabadiliko hayo.

“Wakati nawaambia muziki mgumu haulipi walikuwa wanabisha, wakanitukana, wakiniita majina mabovu lakini nikaja kuwaonyesha mfano kwenye ‘Pombe Yangu’ . Kwahiyo wakaona vile vitu ambavyo mimi navipata, wakaona pesa ambayo naingiza na sasa hivi wao wamebadilika ingawa sio sana lakini hata midundo yao imebadilika,” alisema Madee.

Aliongeza,”Mfano Roma kaimba Singeli, anatafuta hela na yeye, watu kibao tu wamebadilika tunaona beat zimebadilika hata kwa Darassa. Wapo wengi sana hao nimejaribu kuwataja kwa sababu ni watu ambao mimi nipo nao na naamini hawatonielewa vibaya. Ila wengine wanajulikana wao walikuwa wanafanya ngumu lakini wamebadilika wanafanya muziki ambao walikuwa wanaubeza,”

Madee amewataka wasanii wenzake kuacha kufanya hip hop ngumu kwa madai muda wakufanya muziki huo kiharakati ulishapita.

“Mimi wito wangu kwa wasanii ni kuokoa maisha muda wa kuokoa hip hop ulishapita, muziki mgumu utaishia kusifiwa tu unachana lakini hauna lolote katika maisha yako hata vijana wanaokusifia hawanunui kazi zako,” alisema Madee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents