Burudani

Tupac Shakur bado yupo hai – polisi mstaafu

Polisi ambaye ni mstaafu kwa sasa amedai kuwa Tupac Shakur anaweza kuwa bado yupo hai.

Tupac

David Myers, ambaye kwa sasa yupo mahtuti hospitali amedai kuwa alilipwa dola milioni 1.5 kumsaidia rapper huyo kudanganya kifo chake mwenyewe. 2Pac alipoteza maisha baada ya kupigwa risasi mwaka 1996 alipokuwa na umri wa miaka 25.

Lakini sasa Myers anasema anataka ulimwengu ujue ukweli kutoka kwenye kitanda chake anakokaribia kufia. “Ulimwengu unahitaji kujua nilichokifanya. Ninaona aibu kuwa niliacha fedha iathiri maneno yangu, na siwezi kufa bila ulimwengu kujua.”

Anadai kuwa Suge Knight ambaye kwa sasa yupo jela akisubiri hukumu ya mauaji alihusika kwa kiasi kikubwa kwenye mipango hiyo. Watu zaidi ya 30 walidaiwa kulipwa kusaidia kudanganya kifo hicho wakiwemo polisi, madaktari na mashuhuda.

September 7, 1996, Shakur alipigwa risasi kadhaa akiwa barabarani huko Las Vegas, Nevada. Alikuwa kwenye pambano la ngumi kati ya Mike Tyson na Bruce Sheldon.

CHANZO: MIRROR.CO.UK

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents