Habari

Tusamehe Oprah: Switzerland yampigia magoti baada ya kubaguliwa kwa rangi yake kwenye duka la urembo

Nchi nzima ya Switzerland inahaha kumuomba msamaha Oprah Winfrey baada ya muuza duka na mbaguzi mmoja wa rangi huko Zurich kugoma kumuuzia mkoba kwasababu alihisi asingeweza kumudu bei yake.

oprah

Tukio hilo lilitokea mwezi uliopita baada ya Oprah kwenda Zurich kuhudhuria harusi Tina Turner.

Alienda kwenye duka la urembo la Trois Pomme ambako aliona mkoba huo uliokuwa ukiuzwa kwa $38,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 60.

switzerland-trois-pommes-oprah-winfrey

Alipoomba auone, muuza duka huyo aligoma kwakuwa alikuwa na uhakika kuwa Oprah hawezi kuwa na hela hiyo.

“Nijaribu tena, nilisema ‘nataka kuuona huo, na muuza duka akasema, ‘Ohh sipendi kuumiza hisa zako’ na mi nikasema ‘Haya asante sana. Huenda upo sahihi siwezi kumudu bei.’ Na nikaondoka,” Oprah aliiambia Entertainment Tonight.

Na sasa bodi ya utalii ya Switzerland imeomba msamaha kwa niaba ya nchi nzima. Bodi hiyo pia ilimuomba msamaha Oprah Twitter.

Jana Oprah alitweet:

TMZ wamechombeza kwa kuandika: FYI — Oprah reportedly made $77 million dollars last year … so, suck on that racist shop assistant.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents