Habari

Tusicheze na jeshi la polisi wala waandishi – Serikali

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema kwamba,uhalifu wa aina yoyote utakao fanywa na mtu yoyote wa chama chochote, dhidi ya raia yoyote ikiwemo waandishi wa habari na Jeshi la Polisi, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naibu Masauni ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali lililohoji,

je”, Ni juzi tu hapa nimetoka kwenye uchaguzi mdogo Ifakara tarehe 23 ambapo kwanza Mwandishi wa Mwananchi, Juma Mtanda alitekwa na wanachama na wafuasi wa CCM wakampora Ipad, wakampora simu, wakampora na kamera, matokeo yake Polisi wakawatafuta watu wa CCM na wakamrudishia vifaa vyake. maana yake Polisi wanawajua waliofanya uhalifu huu, lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika, hakuna kesi hakuna chochote, lakini kwenye uchaguzi ule askari alipigwa na tofali kapasuka ameshonwa nyuzi tano na amepigwa na wanachama wa CCM lakini Polisi wana muachia anatembea anafanya chochote, sasa naomba waziri aniambie kama CCM wanaruhusiwa kufanya vurugu kutaka kujeruhi askari wetu alafu wakaachiwa huru, naomba nijibiwe.

Akijibu swali hilo, Mheshimiwa Masauni alisema, “Mheshimiwa Lijualikali anazungumzia tuhuma za CCM kuwajeruhi askari Polisi lakini pia kupora waandishi wa habari, Mheshimiwa Naibu spika kwanza kabisa nashindwa kulijibu suala hili moja kwa moja, kwasababu unapozungumzia tuhuma ni kwamba hawa ni wafuasi wa chama fulani inahitaji uthibitisho, ninachoweza kusema uhalifu wa aina yoyote utakao fanya na mtu yoyote wa chama chochote dhidi ya raia yoyote ikiwemo waandishi wa habari na Jeshi la Polisi ndiyo kabisa maana jeshi la Polisi lipo hapa kwaajili ya kulinda usalama wetu hatutakubali kamwe.”

“Mtu yoyote asicheze na Jeshi la Polisi na sio tu jeshi la Polisi hata waandishi wa habari, wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana ya kuweza kuhabarisha jamii na kutoa taarifa nzuri kwa umma. Hivyo hatuwezi kukubali waandishi wa habari au Jeshi la polisi kuweza kufanyia matukio yoyote ya kihalifu na raia mwingine yoyote tutachukua hatua kali za kisheria, kwahiyo muheshimiwa mbunge kama una ushahidi wa hilo jambo ulete kwahiyo siwezi sema chama fulani kimefanya jambo fulani bila uthibitisho.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents