Michezo

Tusker Challenge Cup 2010

Tusker Challenge Cup 2010

 

Mashindano ya Tusker Challenge Cup 2010 yanatarajia kuanza Novemba 27 mwaka huu ikiwa timu 12 zimethibitisha kushiriki katika mashindano hayo.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati SECAFA Bw. Nicolas Musonye alizundumuza na waandishi wa habai leo jijini Dar es Salaam  katika Hotel ya New Africa na kusema kuwa  maandalizi yameshakuwa tayari na nchi  kumi na mbili zimethibitisha ambazo ni watoto wa nyumbani Tanzania, Burundi, Somalia, Kenya, Ivory Coast, Zambia na Malawi. wengine Uganda, Somalia, Zanzibar, Ethiopia, Sudan.

Tusker Challenge Cup 2010

Huku Timu ya Tanzania ikifungua dimba dhidi ya Zambia na Burundi dhidi ya  Somalia. Mtendaji Mkuu wa SBL Bw. Richard Wells amesema SBL itahakikisha timu zote zinapewa huduma zote muhimu wakati zitakapokuwa hapa nchini kwa ajili ya mashindano ikiwa ni pamoja na Chakul, Mlazi na Usafiri wa ndege.

Pia  Mr. Wells aliongezea kwa kusema kuwa mshindi wa kwanza atajipatia dola 30.000, mshindi wa pili dola 20.000 huku mshindi wa tatu akijinyakulia dola 10.000.

Kampuni ya Serengeti Breweriers ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano ya Tusker Challenge Cup.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents