Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Tutaendelea kuvifungia vituo vya mafuta – TRA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa licha ya kufungia mamia ya vituo vya mafuta nchi nzima, leo itaendelea na operesheni hiyo ya kufunga vituo vingine vya mafuta ambavyo havijafunga moja kwa moja mashine za malipo za kielektroniki (EFDs) na pampu.

Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Elijah Mwandumbya

Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Elijah Mwandumbya amesema kuwa waliofungiwa vituo vyao vya mafuta, watafunguliwa tu iwapo watakidhi vigezo ambavyo ni pamoja na kulipia mashine na kuingia makubaliano na mamlaka na TRA.

Tunatoa mwito kwa wale ambao tumeshawafungia wafuate vigezo ili waweze kufunguliwa, wakalipie na waingie na makubaliano na TRA mkoa kwamba ni lini watafunga mashine baada ya kuzilipia,”, amesema Mwandumbya.

Mwandumbya amesisitiza kuwa kwa sasa TRA haitaruhusu wenye vituo vya mafuta waendelee kutumia mashine za mkono ambazo ziko nje ya Pampu kwani wametumia mwanya huo kwa muda mrefu kukwepa kodi ya serikali.

Kamwe hatutaruhusu wafanyabiashara waendelee kukwepa kodi kwa kisingizio cha wananchi kuteseka kwa kukosa huduma, tunachotaka wafuate sheria ya kufunga mashine za EFDs kwenye vituo vyao”.

Akifafanua ulipaji uliokuwa unatumika awali Mwandumbya amesema kati ya watu 10 waliokuwa wakijaza mafuta ni wawili tu ndio waliokuwa wanapewa risiti tena kwa kuzidai.

Hata hivyo TRA inaendelea na operesheni ya kukagua na kufungia vituo vya mafuta vinavyoendelea kukaidi agizo hilo la kununua na kufunga mashine za EFDs.

Kwa Dar es Salaam peke yake tumeshafungia vituo 71, leo tunacompile (tunakusanya) takwimu za nchi nzima na tutatoa taarifa kwa vyombo vya habari,”amesema Mwandumbya.

Chanzo:HabariLEO

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW