Burudani

Tuurudisheni UKIMWI mdomoni – Mrisho Mpoto

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amesema ni vema jamii ikaendelea kuzungumza juu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwani kuna kizazi kilichokuja hivi karibuni hakina uelewa juu ya ugonjwa huo.

Mrisho Mpoto

Akizungumza katika kipindi cha Joto la Asubuhi cha E FM, Mpoto amesema licha ya kuuzungumzia Ukimwi kama njia ya kukumbushana bado upo, pia watu waache mazoea ambayo yanaweza kupelekea maambukizi mapya.

“Elimu itolewe watu waelewe, ndio maana nikasema tuurudisheni Ukimwi mdomoni, tunavyozungumza hivi watu wanakumbuka, unajua hapa katikati tumeacha kuzungumza Ukimwi muda mrefu na kuna kizazi kikubwa sana kimekuja hapa katikati, watoto wamekua hawakuwa na taarifa,” amesema Mpoto.

“Mazungumzo kwenye vipindi mbalimbali yamepotea na watu wamefanya mazoea, mtu sasa hivi anaenda dukani vizuri kununua kondomu akafika kule ndani kuna kitu wanaita ishara… anasema, eeh Mungu nisaidie,” ameongeza.

Msanii huyo amesema sehemu ambazo maambukizi ya Ukimwi yamekuwa juu ni zile ambazo watu wamepuuzia lakini jamii inatakiwa kuzungumza ili watu wajue bado upo na unaendelea kumaliza watu.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents