Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Tuweke kiki pembeni tufanye muziki, wasikilizaji wameanza kuchoka – Wakazi

Rapa Wakazi ni moja ya rappers ambao hawataki kuamini kwenye mambo ya kiki katika kuboost ngoma za wasanii bali anaamini muziki mzuri unaweza kufanya vizuri hata bila ya kiki.

Wakazi

Wakazi amesema kuwa kwa sasa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wanafanya vioja kiasi kwamba hata mashabiki wanajua ni kiki kuna wimbo unatoka.

“Tuweke kiki pembeni tufanye muziki, nadhani muziki ndiko unakoelekea hata raia wanaosikiliza muziki na kuufuatilia wameanza kuchoka sasa. Kwa sababu unakuta mtu kafanya vioja hadi unajua kuwa hii sasa single inakuja,”ameeleza Wakazi kwenye mahojiano yake na Times FM kwenye kipindi cha Playlist.

“Halafu angalia sometimes mambo ya kiki yanavyokuwaga mabaya, inawezekana ikaleta shop value ile unayohitaji ili watu wasikilize bidhaa yako halafu baadae unakuta watu wanaizungumzia kiki yako kuliko hata wimbo wako, wakati wewe unataka wimbo uzungumziwe ili upate show,”amesema Wakazi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW