Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Tuzo za MO Simba kufanyika jioni ya leo

Kwa mara ya kwanza wapenzi wa klabu ya Simba watashuhudia ugawaji wa tuzo maalum kwa watu waliyo saidia timu hiyo kufikia mafanikio yaliyonayo zinazojulikana kwajina la Simba Mo Awards zitakazo fanyika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zilizoanzishwa na Mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji zitakuwa na vipengele 16 ambavyo wachezaji wa Simba waliyofanya vizuri kulingana na nafasi zao baadhi ya viongozi wa klabu hiyo pamoja na mashabiki wakitarajiwa kujinyakulia tuzo hizo.

Wakati lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kutambua mchango wa wachezaji, viongozi na mashabiki ambao juhudi zao zimeiwezesha timu hiyo kupata mafanikio iliyonayo hivi sasa.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW