Tuzo za Wanafunzi

Hii ni kwa mara ya kwanza kabisa nchini kushuhudia tuzo za elimu zikitolewa kwa
wanafunzi waliofanya vizuri kwenye ngazi za shule za msingi pamoja na sekondari na
katika utoaji huo wa tuzo wanamuziki mbalimbali ambao ni Profesa Jay, QJ na
Makamua, Tundaman, Spark pamoja na kundi zima la Bongo Dar-Es-Salaam wakiwemo
kusindikiza utoaji wa tuzo hizo mwezi ujao ndani ya viwanja vya Leaders.

Tumezoea kusikia tuzo zinatolewa kwa wanamuziki bora,waigizaji bora wachezaji bora
na tuzo nyingine mbalimbali lakini kwa hapa nchini hatujawahi kusikia tuzo
zinatolewa kwa wanafunzi bora nchini lakini kwa mara ya kwanza PTECHS inakuletea
tuzo kwa wanafunzi bora nchini ambazo zitakuwa na lengo moja kuu na la muhimu la
kutaka kuwapa moyo wanafunzi ili waweze kufanya vizuri na kuinua elimu nchini.

Mmoja wa waandaaji wa tuzo hizo za elimu,Godfrey Maginga alisema kwamba yeye pamoja
na wenzake waliweza kukaa chini na kujiuliza maswali kwanini kila siku zinaibuka
tuzo mbalimbali na elimu inakuwa inapewa kisogo na ndiyo maana wameamua kuchukua
uamuzi wa kuandaa tuzo hizo maalumu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
Tanzania."Kila siku tunasikia tuzo kwa wasanii mbalimbali lakini hata siku moja
hatujawahi kusikia tuzo kwa wanafunzi ambao ni kizazi chetu cha kesho hivyo ndiyo
maana tuliamua kuandaa tuzo hizi za wanafunzi wanaofanya vizuri nchini"Alisema
Godwin Maganga.

Akielezea kuhusu mchakato mzima wa tuzo hizo,msemaji huyo alisema tuzo haziwezi
kutolewa bila ya burudani yeyote ile hivyo kusindikiza utoaji wa tuzo hizo wameamua
kuwaalika wanamuziki mbalimbali ambao nao watahamasisha wanafunzi kushiriki
mashindano ambayo yanawapelekea kupata tuzo hizo pamoja na burudani.

Bongo5.com iliweza kuongea na baadhi ya wanamuziki hao ambao watatoa burudani siku hiyo
na walisema kwamba ni moja ya changamoto ambayo itaweza kuamsha juhudi za wanafunzi
nchini kufanya vizuri mashuleni. "Kwakweli ni moja kati ya tuzo ambazo zitawapa mwamko wanafunzi wa kusoma kwa bidii ili waweze kupata tuzo hizo" Makamua.

Naye Profesa Jay, mzee wa mitulinga alisema kwamba tuzo hizo ni moja kati ya tuzo
zinazotakiwa kupewa heshima zake nchini kwakuwa ni moja kati ya tuzo ambazo zinaweza
kuibua viongozi wa kesho.

 

Tuzo hizizinatarajiwa kutolewa mwezi ujao tarehe 23 ndnai ya viwanja vya Leaders.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents