Burudani

Twanga, Dully ndani ya Mbalamwezi

twanga

African Stars Band “Twanga Pepeta” inataraji kufanya onesho pamoja na msanii Dully Sykes siku ya Jumapili tarehe 12-06-2011 katika Beach ya Mbalamwezi.
onyesho hilo linataraji kufanyika mchana kuanzia saa nne asubuhi kwa kuwa Twanga Pepeta inataraji kufanya onyesho usiku katika ukumbi wT.C.C kama kawaida.


Kwa wiki hii Twanga haitofanya onyesho katika Bonanza linalofanyika kila Jumapili kutokana na Viwanja vya Leaders kuwa na shughuli maalum ya michezo ya Basketball siku hiyo.

badala yake tumehamishia kwa wiki hii Bonanza katika Beach ya Mbalamwezi na kumshirikisha msanii Dully Sykes ili aweze kuongeza burudani kwani mategemeo yetu ni kuvuta mashabiki wa aina nyingi wakiwemo mashabiki wa Dully Sykes.

baada ya onyesho hilo Twanga Pepeta baadae usiku itamalizia kutoa burudani Katika ukumbi wa T.C.C Changombe kwa kuwatambulisha Vimwana kumi walioingia Fainali katika Shindano la Kumtafuta Kimwana wa Twanga Pepeta 2011.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents