Videos

Twanga Pepeta: Fasha Joshua kuziba pengo la Lilian Internet

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=o4e4DqB9u44[/youtube] Mwanamuziki aliyekuwa ziarani Dubai, Fasha Joshua amerudi upya katika bendi yake ya Twanga Pepeta. Fasha ataziba nafasi iliyoachwa na mwanadada ambaye alikuwa mnenguaji wa kundi hilo Lilian Internet ambaye kwa sasa ameamua kuhamisha makazi yake hadi Mashujaa Band kwa kina Chaz Baba.

Mnenguaji bomba Fasha Joshua
Kiongozi wa kundi la Twanga amesema amepokea taarifa za kuhama kwa mnenguaji wake huyo, lakini kwao haikuzuru kwakuwa tayari wanaye mnenguaji mwingine ambaye alikuwa likizo Uarabuni. Uongozi wa ASET wamesema mnenguaji wao ameanza kazi rasmi Jumatano iliyopita, hivyo taratibu kazi zake zitaanza kuwa wazi mbele ya mashabiki wake.

African Stars Entertainment Tanzania (ASET) aka Twanga Pepeta

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents