Burudani

Twanga sasa kupimana ubavu na Chaz Baba mahakamani

Twanga_Pepeta_Katikati_Asha_Baraka_Akiongea_na_waandishi_wa_Habari_Kuhusu_Uzinduzi_na_Ziara_UK

Katika kuondoka mwanamuziki Chaz Baba Bendi ya twanga pepeta imesema kwamba  haitambui kuondoka kwake kwakuwa hawajapata barua wala taarifa yoyote kutoka kwake kwakuwa mwanamuziki huyo bado wanamkataba naye.

Meneja wa ASET  inayoimiliki bendi hiyo Hassan Reheni, amesema msanii huyo walikuwa wakisaini naye mkataba kila baada ya miaka mitatu, na mkataba wa mwisho amesaini 2011. Hivyo amesema kutokana na kuvunja mkataba huo pasipo kutoa barua kwa uongozi, wala taarifa yoyote basi watahakikisha wanapata haki hata kwa kwenda mahakamani.

Rehani amesema kwamba ingawa anatangaza kwamba hajafanyiwa chochote jambo ambalo si kweli, kwani wamemfanyia mipango mingi ikiwemu kumfanya ajulikane na watu wengi katika tasnia ya muziki wa dansi.

Amesema kwamba walimtoa katika bendi ya Sot Sound akiwa hajulikani hata kidogo, wakamnoa na kumfundisha muziki ikiwemo kuipa jina la albamu ya kumi na moja jina la wimbo wake ingawa haukuwa na maana.

CHAZ_BABA_2
(Chaz Baba akiwa na meneja wake mpya Benard Msemwa katika utambulisho, wa kuahama bendi ya Twanga pepeta)

Pia amesema kwamba mikakati mingi ya kuingusha bendi hiyo tayari wameishaijua, kwakuwa kuna watu wanachuki na bendi hiyo hivyo wamejipanga kwaajili ya kujiimarisha zaidi.

Hassan anasema mikakati yao imeshindwa kwakuwa wao wapo kama timu, na hawategemei mtu kwamba akitoka ndiyo timu ishindwe kufanya kazi. ila wataendelea kufanya kazi kwa pamoja bila ya hofu na mashaka yoyote.

Amesema pia kwao hilo ni funzo, na kuanzia sasa wataweka mikakati kila msanii anayeingia na kukuzwa basi akihama lazima na kampuni nayo ipate faida kama ilivyo kwenye timu za mipira.

 Chzi_baba_Nssf
Twanga wanasema kitambulisho cha NSSF ni miongoni mwa vithibitisho kwamba mwanamuziki huyo ni mali ya Twanga, kwakuwa wasingeweza kuunganisha kama angekuwa hana mkataba.

Bongo5 tupo kuhakikisha tunaona nani ni nani? (Tunafuatilia mkataba kama tutafainikiwa kuuona na kuuleta kwenu)… Unaona utamuuu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents