Michezo

Twitter, Facebook zafuta akaunti za Trump, YouTube yachukua hatua

Akaunti za Twitter na Facebook za rais wa Marekani Donald Trump zimefutwa kwa muda baada ya kutuma ujumbe kwa wafuasi wake waliovamia bunge la Marekani.

Facebook and Twitter remove 'racist baby' video posted by Trump - CNET

Katika ujumbe uliotumwa katika mitadao hiyo kwa waandamanaji, alisema:‘Nawapenda’ akiwataka kwenda nyumbani.

Pia alizungumzia kuhusu madai ya uongo kuhusu udanganyifu uliofanyika katika uchaguzi huo.

Twitter ilisema kwamba inahitaji kuondolewa kwa jumbe tatu za twitter za rais huyokwa kukiuka maadili.

Kampuni hiyo ilisema kwamba akaunti ya rais huyo itasalia kufungwa kabisa iwapo jumbe hizo za twitter hazitaondolewa.

Iliendelea kusema ukiukaji wa sheria za twitter siku zijazo utasababisha kufutiliwa mbali kwa akaunti ya @realDonaldTrump account”.

Hatua hiyo ina maana kwamba siku za Donald Trump katika mtandao wa twitter zitakuwa hatarini.

Rais huyo hajulikani kwa kuheshimu masharti ya muongozo wa twitter kuhusu jamii. Wakati huohuo facebook ilimfuta bwana Trump kwa saa 24 . Wakati huo huo You Tube amechukua hatua za kuiondoa video.

Facebook ilisema: Tuliiondoa kwasababu tuliamini kwamba inachochea badala ya kupunguza ghasia zilizokuwa zikiendelea.

Wafuasi wake walivamia kiti cha serikali ya marekanina kukabiliana na maafisa wa polisikitu kilichosababisha kifo cha mwanamke mmoja.

Ghasia hizozilisitisha mjadala kuhusu ushindi wa rais mteule Joe Biden.

Kabla ya ghasia hizo rais Trump aliwaambia wafuasi wake mjini Washington kwamba uchaguzi huo uliibwa.

Saa chache baadaye ghasia kuzuka ndani na nje ya jumba la Capitol Hill , alionekana katika video akirejelea madai hayo ya uongo.

You tube ilisema kwamba iliiondoa kanda hiyo ya video kwasababu ilikiuka seraza kusambaza madai ya udanganyifu kuhusu uchaguzi uliopita.

Awali twitter haikuwa imeiondoa video hiyo , na badala yake kuondoa uwezo wake wa kujibiwa , kupendwa na kutolewa maoni. Lakini baadaye iliiondoa na kufuta akunti ya rais huyo anayeondoka madarakani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents