Habari

Twitter imeanzisha mfumo wa kutoa tahadhari kwa watumiaji wake kipindi cha dharura na majanga

Mtandao wa kijamii wa Twitter umeanzisha mfumo wa tahadhari kwa kuwaarifu watumiaji wake juu ya dharura na majanga pindi yanapojitokeza katika nchi zao.

An illustration picture shows a Twitter blue bird symbol on an Ipad, in Bordeaux

Watumiaji wa Twitter ambao watajisajili kupata huduma hiyo watapokea ‘notification’ kupitia Twitter app pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi katika simu zao za mkononi.

Ili kupata taarifa kupitia simu za mikononi watumiaji watalazimika kutoa namba zao za simu kwa mashirika ambayo yanasimamia mpango huo.

Kwa mujibu wa Reuters, Twitter wamesema mfumo wa tahadhari utasaidia watumiaji kupokea ‘alerts’ kutoka vyombo vya serikali pamoja na mashirika ya misaada wakati wa dharura yoyote.

Miongoni mwa mashirika ambayo tayari yamesaini ni Shirika la Afya Duniani (WHO).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents