Technology

#TwitterGulio : Kwa sasa unaweza kununua/kuuza bidhaa mbalimbali kupitia Twitter

Kama upo Tanzania na ni mtumiaji mzuri wa mtandao wa Twitter basi sahau adha za kutembea masokoni au kwenye maduka kusaka bidhaa kwani kuna gulio limeanzishwa kwenye mtandao huo unaotumiwa na zaidi ya watumiaji milioni 350 duniani kote.

Je, utawezaji kutafuta bidhaa unayoitafuta?

Jibu ni kwamba utaandika hashtag ya #TwitterGulio kwenye Search Engine ya Twitter na kisha utaona bidhaa zote zilizowekwa sokoni kwa siku hiyo, zikiwa zimeambatanishwa na Bei, Mawasiliano, na Picha na maelezo mengine muhimu kuhusu bidhaa husika.

Akizungumza na Bongo5 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ubora Business Consultancy, Ndugu Lameck Isaya amesema Lengo kubwa la #TwitterGulio ni kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo kutangaza bidhaa zao bure mtandao .

Twitter Gulio ni jukwaa la mtandaoni ambalo linawapa fursa wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati kutangaza bidhaa zao kupitia mtandao wa Twitter ambapo itamlazimu mjasiriamali kuweka picha/video ya bidhaa yake, Sifa ya bidhaa na Mawasiliano yake ya namba za simu ili kuwasiliana na mteja atakayepatana naye.“amesema Isaya.

Hata hivyo, Isaya amesisitiza kuwa Twitter Gulio itakuwa platform nzuri kwa wajasiriamali na itapunguza gharama kwa wanunuzi kwani mteja atawasiliana na muuzaji moja kwa moja bila kupitia kwa madalali.

Twitter Gulio itakuwa inafanyika kila siku za ijumaa, na hakuna gharama zozote kujiunga kwa wajasiriamali watakaohitaji kutangaza bidhaa zao, cha kuzingatia ni kukumbuka kuweka Hashtag ya #TwitterGulio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents