Habari

Two kings working together: Timberland kutengeneza nyimbo mpya za Michael Jackson

Tegemea kupata nyimbo mpya za mfalme wa Pop duniani Michael Jackson siku za karibuni zitakazokuwa na ladha ya midundo ya producer mkongwe Timberland.

timberland

Timothy Zachery Mosley a.k.a Timberland amesema yuko jikoni akikamilisha project ya nyimbo za mfalme wa Pop duniani marehemu Michael Jackson. Katika video clip fupi Timberland amefafanua kuwa MJ aliwahi kwenda na kuzungumza naye kuhusu kufanya naye project ambayo producer huyo ameiita “two kings working together” yaani MJ akiwa mfalme wa Pop na Timberland akiwa mfalme wa midundo.

michael-jackson2

Timberland amesema ‘Chicago’ ndio itakuwa single ya kwanza ya Michael Jackson kutoka katika project hiyo ambayo itakapokamilika itakuwa na sauti za MJ zitakazokaa juu ya midundo ya muandaaji huyo.

Tarehe kama ya leo (August,29 1958) ndiyo alizaliwa mfalme wa Pop duniani Michael Joseph Jackson, na alifariki dunia (June 25, 2009)

Msikilize Timberland akiizungumzia project hiyo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents