Burudani

Tyga kutumia style mpya kwenye albamu yake ijayo

By  | 

Unatarajia kusikia kitu gani kwenye albamu mpya ya Tyga? Basi kuna uwezekana mkubwa ukasikika style mpya ambayo hujawahi kuisikia kutoka kwa rapper huyo.

Msanii huyo amezoeleka kwa kuchana zaidi kwenye ngoma zake lakini katika albamu yake mpya itakayotoka hivi karibuni tegemea kumuona msanii huyo akiimba zaidi.

Tyga amewashtua mashabiki baada ya video kusambaa mitandaoni ikimuonyesha Tyga akiimba nyimbo ya Usher Raymond na Donell Jones kitendo ambacho kimezua maswali mengi.

Baada ya tukio hilo, rapper huyo kupitia mtandao wake wa Twitter ameandika, “Y’all think I’m playing that singing album coming soon?.”

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments