Michezo

Tyson amtwanga vibaya Deontay Wilder ”Mfalme amerejea kwenye kiti chake” (+Video)

Tyson alionyesha umahiri wake katika ulingo baada ya kumaliza ufalme wa Deontay Wilder wa miaka mitano na kuchukuwa mkanda wa WBC katika uzani mzito duniani baada ya kumwangusha binngwa huyo kwa njia ya knockout katika raundi ya saba.

https://www.youtube.com/watch?v=1VfWQOzUa9U

Katika mechi iliochezewa katika Mecca ya ndondi mjini Las Vegas nchini Marekani raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 31 alimshinda mpinzani wake katika pigano ambalo ni wachache wangeweza kutabiri..

Mchanganyiko wa ngumi za kulia na kushoto ambazo Wilder amekuwa akizitumia kuwalambisha sakafu wapinzani wake zilitumika dhidi yake na kuangushwa katika raundi ya tatu na tano.

Fury alihakikisha ametimiza aliyoahidi na kubadili mbinu zake kutoka upigaji hadi mwenendo wake na kumzidia nguvu mpinzani wake ambaye hajawahi kushindwa.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Tyson ameandika: “Nataka kusema Deontay Wilder, ameonyesha weledi wake. Amepigana hadi raundi ya saba. Yeye ni shujaa, atarejea tena kuwa bingwa. “Lakini mfalme amerejea katika kiti chake.”

Je huu huu utakuwa ni wakati wa mwisho Deontay Wilder kuwa kwenye mpambano? Amekuwa bingwa wa dunia tangu january 2015.

Je atajaribu tena kurejesha taji lake? ama pengine mambo kwenda mrama katika raundi ya saba kutahitimisha taaluma ya raia huyu wa Marekani?

Tyson Fury ametimiza kile alichosema atafanya na kile ambacho wengi walikuwa na mashaka ikiwa anaweza kutimiza.

Alitawala pambano hilo na kuonyesha kwanini alihitaji sana kuongeza uzito na pia sababu ya yeye kubadilisha makocha kila mara.

Tyson Fury na Deontay Wilder

Kidogo tu Wilder aishie kula mangumi usiku mzima.

‘Natarajia pigano la tatu’

Tyson Fury akizungumza na BT Sport: “Nilimwambia kila mmoja kwamba mfalme anarejea kwenye kiti chake. katika pigano langu la mwisho karibu kila mmoja alinikashifu. Nilikuwa na uzani wa chini na nilifanya mazoezi kupitiza. Mimi ni muharibifu. lakini sio vibaya kwa mwanamasumbwi.

“Natimiza ninachosema. Nilimwarifu Wilder, timu yake, na dunia nzima. Tulifanya mazoezi ya knockout.

“Ninazungumza hivi kwasababu ninaweza kutoa ushahidi wa ninachokizungumzia. Watu walinisema vibaya, waliangalia kitambi changu na upara wangu na kudhania kwamba siwezi kupigana. Alipigana kwa weledi kadiri ya uwezo wake wote Tyson Fury na kila mmoja yuko katika kipindi chake cha juu.

“Namtarajia [Wilder] aombe pigano la tatu. najua kwamba yeye ni shujaa na mimi nitakuwa na msubiri.”

Fury kisha akasema kwamba anataka pambano la tatu dhidi ya Wilder lifanyike uwanja wa Las Vegas ambao kwa sasa unajengwa na utafunguliwa hivi karibuni.

Tyson Fury

Tyson Fury ‘Natarajia igano la tatu’

Wilder amepelekwa hospitali

Kulingana na mwanishi wa BBC Luke Reddy, Las Vegas

Deontay Wilder, amepelekwa hospitalini hivyo hataweza kuzungumza na wanahabari.

Kulingana na timu yake, Wilder amepelekwa hospitali kushonwa baada ya kujeruhiwa kwenye sikio.Pambano kati ya Tyson Fury na Deontay Wilder

Pambano kati ya Tyson Fury na Deontay Wilder

Historia ya pigano

Tyson Fury, ametawala pambano hilo na kumzidia nguvu haswa katika raundi ya tatu na raundi ya tano.

Kamba za kwenye ulingo ndizo zilizokuwa mkombozi kwa mwanamasumbwi huyo wa Marekani kwa mara ya tatu.

Lakini Furry hakumpa nafasi Wilder kumshambulia.

Mapema kwenye raundi ya saba, alimshambulia tena na wakati huu Wilder na hapo ndipo maji yalipozidi unga Wilder akawa hana la kufanya zaidi ya kusalimu amri huku Fury akiwa bingwa wa dunia katika uzani wa heavy kwa mara ya pili.Tyson Fury akisherehekea ushindi wake

Tyson Fury akisherehekea ushindi wake

Wakati huo huo, Eddie Hearn, msimamizi wa Anthony Joshua ameonyesha kwamba mteja wake yuko tayari kupambana na Fury. ”’Fury dhidi ya Joshua katika msimu wa joto au vuli? pengine. Natumai”.

Eddie Hearn ameandika kwamba hakuna haja ya kwenda kwenye pigano la tatu badala yake moja kwa moja kuandaliwe pigano jipya msimu wa joto ujao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents