Michezo

Tyson Fury anyang’anywa mkanda wa IBF

Bingwa wa ngumi dunia wa uzito wa juu, Tyson Fury amevuliwa mkanda wa IBF ikiwa ni chini ya wiki mbili baada ya kushinda.

2EE3DAA800000578-0-Tyson_Fury_became_heavyweight_champion_of_the_world_beating_Wlad-a-56_1449100672375

Bondia huyo wa Uingereza mwenye miaka 27, mwanzo alitakiwa kukubali kupigana na Vyacheslav Glazkov ili kutetea mkanda huo lakini badala yake amekubali mchezo wa mruadiano dhidi ya Wladimir Klitschko.

Fury alimpiga Klitschko wa Ukraine kwa pointi Novemba 28 mwaka huu na kushinda mikanda mitatu ya uzito wa juu iliyokuwa ikishikiliwa na bondia huyo.

Mwenyekiti wa IBF Lindsey Tucker amethibitisha taarifa hizo akidai kuwa Fury alipaswa kutetea mkanda huo kwa kuzichapa na Glazkov lakini badala yake ameamua kurudiana na Klitschko.

Fury ambaye hajapigwa katika pamano 25, amebakiwa na mikanda ya WBA na WBO wakati mkanda wa WBC ukiwa unashikiliwa na Deontay Wilder wa Marekani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents