Michezo

Tyson Fury kurudiana tena na Klitschko Julai tarehe 9

Pambano la marudio kati ya Tyson Fury na Wladmir Klitschko litaandaliwa mjini Manchester mnamo mwezi Julai tarehe 9 kulingana na mkufunzi wa bondia huyo wa Uingereza.

2EE564EA00000578-3529631-image-a-2_1460104766509

Peter Fury alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter siku ya Ijumaa na tangazo jingine linatarajiwa baadaye.

32F73D5600000578-3529631-image-a-21_1460106958772

Fury ambaye ni mzaliwa wa mjini Manchester na ambaye ana umri wa miaka 27,alimshinda raia wa Ukraine Klitschko kwa pointi mjini Dusseldorf mwezi Novemba ili kushinda mikanda mitatu ya WBA,IBF na WBO.

Ushindi huo unamaanisha kwamba Fury ni Muingereza wa tano kushinda mataji hayo ya uzani mzito zaidi duniani.

Hatahivyo Fury alipokonywa ukanda wa IBF wiki mbili baada ya ushindi huo na marudiano na Klitschko yanamaanisha kwamba hatokabiliana na bingwa wa uzani huo Vyacheslav Glazkov.

Taji hilo litakuwa wazi siku ya Jumamosi ambapo mshindi wa medali ya dhahabu katika shindano la Olimpiki Anthony Joshua atakabiliana na bingwa mtetezi Charles Martin katika ukumbi wa 02 mjini London.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents