Habari

Uamuzi wa Mahakama kesi ya wabunge 8 waliotimuliwa CUF (+Picha)

Mahakama Kuu ya Tanzania, imehairisha kutoa hukumu ya pingamizi liliwasilishwa na wabunge 8 wa Viti Maalum waliotimuliwa CUF la kupinga Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutowaaapisha wabunge wapya walioteuliwa na mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa.

Akizungumza na wanahabari nje ya Mahakama leo Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Mbarala Maharagande anayeunga mkono upande wa Maalim Seif amesema kuwa Mahakama hiyo itatoa maamuzi Agosti 25 mwaka huu.

Maharagande amesema kuwa Mahakama imeona hakuna jambo lolote hapa katikati litakalo weza kuathiri uamuzi unaotarajiwa kutolewa Agosti 25 mwaka huu kabla ya kuapishwa wabunge 8 wapya wanatarajiwa kuapishwa katika bunge litakaloanza tarehe 5,Septemba mwaka huu.

Wabunge wapya walioteuliwa na NEC ni Zainab Mndolwa Amir ,Kiza Hussein Mayeye,Hindu Hamis Mwenda, Rukia Ahmed Kassim,Shamsia Aziz Mtamba, Sonia Juma Magogo,Nuru Awadh Bafadhili na Alfredina Apolinary Kahigi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents