Burudani

Ubachela waanza kumtesa Angelina Jolie

Mara hii tena! Angelina Jolie ameonyesha kuchoshwa na maisha ya kuishi usela.

Muigizaji huyo ambaye aliachana na mumewe Brad Pitt takribani mwaka mmoja uliopita, ameliambia gazeti la Sunday Telegraph, imekuwa ngumu kwake na hafurahii maisha ya upweke ambayo anaishi sasa hivi.

“Imekuwa ngumu. Sifurahi kuwa peke yangu. Sio kitu ambacho nilitaka. Hakuna kitu kizuri juu hilo. Ni vigumu. Labda wakati mwengine inaonekana najilimbikizia kila kitu, lakini kwa kweli najikaza kusukuma siku zangu,” amesema Jolie.

“Kwa kihisia, imekuwa mwaka mgumu sana, na nimekuwa na maswala mengine ya afya. Hivyo afya yangu ni kitu ambacho ni lazima nipate kufuatilia,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents