Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Ubaguzi kuliua TMK Wanaume?

Siku chache baada ya kulalamikiwa kinoma na wadau wa muziki kwa kitendo cha kundi la Wanaume TMK kujitangaza hadharani kuwa linavuta bangi,mdudu mwingine ameanza kulimega kundi hilo.


Siku chache baada ya kulalamikiwa kinoma na wadau wa muziki kwa kitendo cha kundi la Wanaume TMK kujitangaza hadharani kuwa linavuta bangi,mdudu mwingine ameanza kulimega kundi hilo.

Wanaume wa TMK wakiwa kazini.

Mmoja wa wanamsakani wa (TMK Wanaume) aliyeongea na DHW kwa sharti la kutotajwa jina lake alisema kinachotokea sasa hivi ni baadhi ya wasanii wa kundi hilo kuona kwamba hawatendewi haki..na kuhisi kuwa kuna upendeleo wa dhahirimiongoni mwao unaofanywa na uongoziwa kundi hilo.

Mwanamaskani huyo alisema wasanii hao hata hivyo wamekuwa wakishindwa kumlalamikia Manager wao (Said Fela) kwa kuogopa kutemwa ndani ya kundi hilo maarufu nchini,na hivyo kubakia kuongea chichini jambo ambalo haliwasaidii kitu.

Kwa kujaribu kutihibitisha hilo mwanamaskani huyo alisema tayari msanii Kaka Man aliyetamba sana na songo lake (Kama Noma na Iwe noma),amekwishajiengua ndani ya kundi hilo na kuamua kujitegemea mwenyewe na tayari ameshamaliza utengenezaji wa albam yake akiwa hayuko chini ya kundi hilo.

Mpaka tunakwenda mitamboni juhudi za kumtafuta Said Fela ambaye ndiye Manager wa kundi hilo ili atuthitishie kuhusu sakata hili..zilishindikana kutokana na simu yake kuwa busy kila ilipopigwa.

  • SOURCE: Darhotwire

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW