Habari

Ubalozi wa Kuwait watoa msaada wa visima viwili vya maji shule mbili za Mburahati

Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umeendelea na jitihada zake za kuisaidia jamii ya kitanzania ambapo Ijumaa hii umekabidhi visima viwili vya maji safi kwa shule ya msingi Baridi iliyopo kata ya Mburahati pamoja na shule ya secondari ya Mburahati jijini Dar es salaam.

Balozi wa Kuwait Tanzania, Jasen Al-Najem (mwenye kanzu nyeupe kulia) Ijumaa hii akizindua kisima cha maji safi cha shule ya msingi Baridi Mburahati jijini Dar es salaam kilichojengwa chini udhamani wa ofisi yake.

Kabla ya msaada huo shule hizo zilikuwa zinakabiliwa na tatizo la maji hali ambayo ilisababisha kuathiri maendeleo ya wanafunzi hao.

Akiongea wakati wa kukabidhi visima hivyo, Balozi wa Kuwait Tanzania, Jasen Al-Najem amesema visima hivyo vya maji safi vitaweza kuwafanya wanafunzi kusoma vizuri kwa kuwa mazingira yao yatakuwa na maji ya kutosha ambayo watayatumia katika huduma mbalimbali.

“Maji ni huduma muhimu kila sehumu, hii ni huduma ambayo inatakiwa kuwa katika mazingira ya karibu ya shule. Lakini kutokana na changamoto ya maji ambayo mlikuwa nayo tumewajengea hiki kisima ambacho kitakuwa kinatoa maji masafi kwa matumizi yote. Maji ambayo yanatoka hapa ni safi na yanafaa kwa matumizi yote,” alisema Jasen.

Wanafunzi wa shule ya msingi, Baridi wakisikiliza jambo kwa makini

Balozi huyo amesema ataendelea kuwa karibu na shule hizo ili kuendelea kuzisaidia changamoto mbalimbali ikiwemo ya uchakavu wa madarasa pamoja vifaa vya kujifunzia.

“Tunataka kuendelea kuisaidia serikali pamoja na Rais wetu mpendwa Magufuli katika jitihada zake za elimu bure. Kwahiyo tumezisikia changamoto zote, uchakavu wa madarasa, fensi za shule pamoja na mambo mengine ambayo yameelezwa awali,” alisema Jasen.

Kwa upande mwalimu mkuu wa shule ya msingi Baridi, Osdory Kibasa, amesema msaada huo utaweza kuwafanya wanafunzi hao kusoma vizuri.

Diwani wa kata ya Mburahati,Yussuf Omary Yenga (kushoto) akielekeza jambo mbele ya balozi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents