Burudani

Ubalozi wa Marekani walipa shavu Hip-Hop Darasa la Fid Q

September 8 mwaka huu, kaimu afisa wa masuala ya kijamii Roberto Quiroz II na afisa msaidizi wa masuala ya kitamaduni Shamsa Suleiman wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, waliungana na rapper Fareed Kubanda aka Fid Q kwenye Hip Hop Darasa jijini Dar es Salaam lililohudhuriwa na washiriki vijana zaidi ya 100.

Katika ziara hiyo, ubalozi wa Marekani ulilisaidia darasa hilo zaidi ya vitabu 100 na mipira ya kikapu kwa niaba ya watu wa Marekani.

“Tunafundishwa na Fid Q maana halisi ya mafanikio, – kurudisha kwa jamii kwa kuelewa kuwa kila mtu ana thamani kubwa na umuhimu, kuhakikisha kuwa vijana wa leo wanapokea mafunzo na elimu muhimu kwa maisha yao ya baadaye,” alisema Quiroz II.

“We are honored to partner with Fid Q and his team in this noble and urgent endeavor.” books and basketballs on behalf of the American people to participants.”

Fid Q alianzisha mradi huo kuwafundisha watoto, vijana na wale wanaopenda kuwa wasanii kupromote vipaji vyao, kuwapa elimu na kuwaelekeza mienendo sahihi katika jamii wanayoishi.

Darasa hilo huwafundisha vijana kuzungumza masuala mbalimbali kupitia muziki na sanaa na kutoa mitazamo na michango yao kwenye jumuiya zao kwa ushirikiano na kufanya kazi kama timu na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents