Technology

Uber yaja na huduma ya kusambaza chakula Afrika ‘UberEATS’

Kampuni ya Uber, imeanzisha app ya kusambaza chakula, UberEATS nchini Afrika Kusini Jumatano hii.

download

Uber, iliyojipatia umaarufu kwa huduma ya taxi duniani, ina lengo la kuipanua huduma hiyo kwenye nchi zingine za Afrika, ikiwemo Tanzania.

Meneja mkuu wa Uber Afrika, Alon Lits amedai kuwa UberEATS ina nafasi kubwa ya kubadilisha mtindo wa ulaji.

“UberEATS has the ability to change the way restaurants operate. Through partnerships given the scale, smaller businesses could expand to a wider customer base through UberEATS,” Lits aliiambia Fin24.

“While reaching more customers through UberEATS, restaurant owners could now think of investing elsewhere in their businesses, like adding more seats or additional kitchen space,” aliongeza.

App hiyo itatumia mfumo wa Uber ambapo utahusisha madereva washirika kusambaza vyakula kutoka kwenye hoteli mbalimbali. UberEATS, hata hivyo ni app inayojitegemea na ile nyingine ya kukodi usafiri.

Huduma hiyo itaanza kupatikana jijini Johannesburg kabla ya kusambaa kwingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents