Habari

Uchaguzi Burundi: Matokeo ya awali kutangazwa leo 

Tume ya uchaguzi nchini Burundi inatarajiwa kutangaza hii leo, matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumatano iliyopita, huku Evariste Ndayishimiye, mgombea aliyeteuliwa na rais anayeondoka Pierre Nkurunziza akipewa nafasi kubwa ya kutangazwa mshindi. Kulingana na mwaliko wa tume hiyo kwa vyombo vya habari, tangazo hilo la matokeo ya awali litatolewa saa nane mchana majira ya Burundi, na matokeo kamili yatatangazwa Juni 4.
Matokeo ya muda yaliyochapishwa na shirika la habari la taifa yamemuonyesha Ndayishimiye akiongoza na asilimia 80 ya kura zilizopigwa.
Mpinzani wake mkuu, Agathon Rwasa ambaye mikutano yake ya kampeni ilihudhuriwa na umati mkubwa aliambulia asilimia takribani 20, huku wagombea wengine 5, kwa pamoja wakimudu asimilia moja.
Msemaji wa Rwasa amesema kilichotokea ni mpango uliosukwa vyema na chama tawala wa kung’ang’ania madarakani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents