Habari

Uchaguzi Burundi: Tume yawataka wananchi kuwa na subira

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Burundi, Pierre-Claver Kazihise, amewatolea wito wananchi kuwa na subira, huku masanduku ya kura yakiwa yanaendelea kukusanywa na kura zikiwa zinahesabiwa kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa utakaoamua mrithi wa kiongozi wa muda mrefu nchini humo Pierre Nkurunziza.

An election official prepares ballot papers at a voting station during the Presidential, Legislative and Communal council elections in Gitega, Burundi, on May 20, 2020.

Kazihise aliwasihi watu kuwa na utulivu, akisema mchakato wa kuhesabu kura zote utachukua siku kadhaa, na matokeo yatatangazwa Jumatatu au Jumanne.

Kufuatia kampeni zilizogubikwa na vurugu, uchaguzi ulikuwa shwari. Hata hivyo kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha National Freedom Council (CNL), Agathon Rwasa amedai kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi huo na maafisa wake kadhaa walikamatwa.

Tume ya uchaguzi bado haikujibu madai hayo. Uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 uliompa ushindi wa muhula wa tatu Nkurunziza, ulisababisha vurugu zilizopelekea watu 1,200 kuuawa na wengine wapatao 400,000 kuikimbia nchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents