Burudani ya Michezo Live

Uchaguzi FIFA: Ombi la mgombea wa Urais Prince Ali latupiliwa mbali

Ombi la mgombea wa Urais, Prince Ali bin al Hussein la kutaka kuwepo vyumba vya wazi vya kupigia kura kwenye uchaguzi wa FIFA Ijumaa hii limetupitiwa mbali na mahakama ya rufaa ya michezo.

Jordan's Prince Ali Bin Al-Hussein, FIFA's Asian vice president and chairman of the Jordan Football Association, poses for photographers after a news conference in central London

Uchaguzi huo utaendelea kama ulivyokuwa umepangwa. Katika uchaguzi wa May, Sepp Blatter alimshinda Prince Ali kabla ya kujiuzulu siku chache baadaye.

Kwenye maelezo yake baada ya kuamriwa hivyo, Prince Ali alisema: Nimefanya kila kitu nilichoweza. Najuta kwamba mfumo umetuangusha.”

Vyumba sita vya wazi vya kupigia kura vilikuwa vimeshatengenezwa na kuwasili mjini Zurich Jumatano hii lakini havitatumika.

Prince Ali ambaye ni raia wa Jordan anachuana na Sheikh Salman bin Ibrahim al Khalifa wa Bahrain, Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, Tokyo Sexwale wa Afrika Kusini na Jerome Champagne wa Ufaransa.

Wajumbe kutoka zaidi ya nchini 200 watapiga kura.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW