Michezo

Uchaguzi TFF: Ally Mayay atikisa ofisi kuu za TFF (Video)

Katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF unaotarajiwa kufanyika Agust 12 mwaka huu, aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Yanga SC, Ally Mayay amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais.

Aliyekuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya Yanga, Ally Mayay akionyesha fomu yake aliyo chukua TFF

Mayay ameingia katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini huku akiungana na mchezaji mwenzake wa zamani, Mtemi Ramadhan ambaye naye amejitosa kuchukua fomu ya kugombea umakamu wa Rais na kusindikizwa na wapenzi wa soka na baadhi ya wachezaji wazamani akiwemo Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’

Mayay anatarajiwa kuwa, huenda akawa mpinzani mkuu wa Rais anayetetea nafasi yake, Jamal Malinzi

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents