Uchaguzi TFF Wazidi Kunoga

HOMA ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imezidi kupanda kwa viongozi wa Simba, Evarist Hagila kuvaana jino kwa jino na Samwel Nyala, wote wakigombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji kupitia Mkoa wa Mwanza na Mara

HOMA ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imezidi kupanda kwa viongozi wa Simba, Evarist Hagila kuvaana jino kwa jino na Samwel Nyala, wote wakigombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji kupitia Mkoa wa Mwanza na Mara.
Hagila ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa juzi mkoani Mwanza nafasi ya kuwakilisha klabu wakati Samwel Nyala alifanikiwa kutetea nafasi yake ya ujumbe wa mkutano mkuu wa TFF katika uchaguzi huo.
Kujitokeza kwa Hagila kuwania nafasi moja na Nyala kumezua hisia tofauti miongoni mwa wadau wa soka kuwa kuna tatizo kutokana na wagombea hao wote kutoka Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza, ‘MZFA’.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo jana, Hagila alisema: “Nimechukua fomu ili nipambane na Nyalla na nimepata msukumo mkubwa baada ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa MZFA, naamini wajumbe watamchagua yule mwenye sera nzuri,”alisema Hagila.
Hata hivyo, wawili wao wanaungana na Katibu Mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa ambaye amejitosa kuwania nafasi ya makamu wa pili wa rais wa shirikisho hilo, nafasi iliyokuwa ikikaimiwa na Jamal Bayser baada ya Ismail Aden Rage ambaye alikuwa akiishikilia kupata matatizo ya kijinai.
Wagombea wengine ambao jana walichukua fomu ni Amir Roshan anayetetea nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya utendaji kupitia kanda ya Kagera na Shinyanga pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Athuman Nyamlani ambaye anawania nafasi ya Makamu wa kwanza wa rais nafasi ambayo pia inatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na katibu mkuu wa zamani wa TFF Michael Wambura ikitazamiwa kuchukua fomu leo kuwania nafasi hiyo.
Kujitokeza kwa wagombea hao jana kumefikisha idadi ya wagombea 13 ambao ni Leodegar Tenga, Richard Lukambura, Jamal Malinzi (rais), Ismail Rage, Samwel Nyala, Shaibu Nampunde, Wallace Karia Eliud Mvela, Amir Roshan, Evarist Hagila (ujumbe), Athuman Nyamlani, Lawrence Mwalusako (makamu wa kwanza wa rais), na Lucas Kisasa (makamu wa pili wa rais).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents