Michezo

Uchaguzi wa Simba wapigwa ‘stop’ na TFF

Kamati ya uchaguzi ya TFF imetangaza kuupiga stop uchaguzi mkuu wa Simba kutokana na sababu mbalimbali za kisheria.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF Wakili Revocatus Kuuli amezitaja dosari ambazo wamezibaini katika mchakato wa uchaguzi wa Simba.

“Ni kweli tumesimamisha mchakato huo ili wafanye maboresho kwa changamoto tulizoziona kama kamati halafu baadaye wataendelea na taratibu za uchaguzi. Zipo dosari kubwa ambazo ni za kisheria, mchakato wao haujaweka matakwa ya kisheria kama kuhusishwa kamati ya rufaa, kamati ya maadili, kanuni inayotumika siyo ambayo inatakiwa.” alisema Wakili

Aliogeza,”Wao wanatumia kanuni za uchaguzi za TFF lakini walitakiwa watumie kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF, pia kutumia kanuni tofauti kumeleta usumbufu kidogo katika tafsiri. Kanuni za wanachama zinataka mgombea wa nafasi ya mwenyekiti achukue fomu kwa shilingi 200,000 na nafasi nyingine 100,000 lakini kamati ya Simba wao wameamua kuweka kiwango kikubwa cha shilingi 500,000 kwa madai kwamba wanatumia kanuni za uchaguzi za TFF kitu ambacho kikanuni hakitakiwi kuwa hivyo. Wakiweza kurekebisha dosari tulizozibaini wanaweza kuendelea na mchakato wao vizuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents