Michezo

Uchambuzi: Ally Mayai aipa Madrid ubingwa UEFA leo (Video)

Ikiwa hii leo Dunia itakaa kimya kwa muda kushuhudia michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya katika mchezo wa fainali unao wakutanisha mabingwa wa tetezi wa kombe hilo na mabingwa wa ligi kuu nchini Hispania, Real Madrid  dhidi ya  mabingwa mara tano mfululizo wa Italia, Juventus mjini Cardiff.

Bongo5 imezungumza na mchambuzi wa soka nchini na mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa na klabu ya Yanga, Ally Mayai ‘Tembele’ kuelekea mchezo huo wa fainali.

Mchambuzi wa mpira wa miguu nchini, mchezaji wa zamani wa Taifa ‘Taifa Stars’ na klabu ya Yanga, Ally Mayai ‘Tembele’.

“Fainali yoyote  ya Uefa ni moja kati ya mechi kubwa kuliko  mechi nyingine zozote  ukiachiliambali fainali za kombe la Dunia, kwa sababu ndio michezo ambayo inaingiza fedha nyingi na hata bingwa anapata fedha nyingi kuliko bingwa wa kombe la Dunia”.

“Wale walioshiriki tu hata Leicester City wamepata zaidi ya  Euro 34 m,  kwahiyo unaweza kuona jinsi ambavyo atakae shinda atapata kiasi gani cha fedha hiyo yenyewe ni moja  kati ya sababu tosha ambazo zinazofanya mechi hizi kuwa kubwa na kufuatiliwa na watu wengi”.

“Ukizungumzia Real Madrid na Juventus unazungumzia timu mbili ambazo zote zinahistoria tofauti na zina aina ya wachezaji ambao kila kocha anajivunia, mfano Juventus kocha anajivunia kikosi cha wachezaji ambao ni wazoefu. Kwa kawaida msingi wa timu huwa unajengwa na wachezaji wazoefu”.

“Kocha Zinedine Zidane wakati anaingia Real Madrid hakuwa akiaminika sana kwa sababu ametoka katika timu ya vijana ya Castilla, alipofika bahati nzuri msimu wa kwanza alifanikiwa kuchukua Uefa Champions League akicheza dhidi ya Atletico Madrid kupitia mikwaju ya penati wakati  Cristiano Ronaldo alipo walaza watani zao na amethibitisha mpira ni sayansi”.

“Kwa hiyo ni sayansi ambayo mwalimu Zinedine Zidane na kweli akathibitisha kuwa licha ya uchanga aliokuwa nao katika kufundisha mpira amefanya watu waanze kumfikiria kama wakina Pep Guardiola ama Jose Mournho, kwahiyo wanaingia leo  Real Madrid  wanataka  kuweka  rekodi kwasababu siku zote wamezoea  kufanya  hivyo, toka Uefa Champions League ianze hakuna timu iliyowahi kushinda ‘back to back’ na kutetea tena taji hili kwa mara ya pili”.Alisema Ally Mayai

Klabu hizo zimekutana mara 18,Juventus wakishinda nane na Real Madrid nane, wakitoka sare mbili.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents