Habari

UCHAMBUZI: Kilichomuangusha Trump, mambo atakayokabiliana nayo Rais Joe Biden (+Video)

Joe Biden Rais wa 46 wa taifa la Marekani aliyeapishwa Jumatano ya wiki hii baada ya kufanikiwa kuingia White House kwa kumshinda rais aliyekuwa madarakani Donald Trump katika uchaguzi.

Kuangalia video bofya HAPA

Biden, ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Marekania wakati wa utawala wa Barack Obama, anarudi Ikulu na jukumu la haraka la kushughulikia mgogoro wa kiafya na kiuchumi vinavyosababishwa na janga la virusi vya corona.

Mwanachama huyu wa Democratic mwenye umri wa miaka 78 alichukua madaraka siku ya Jumatano katika hafla isiyo ya kawaida kwa sababu ya hatua kubwa za usalama ambazo zilipitishwa kuzuia mashambulio na uwezekano wa kutokea vurugu.

Akiwa Rais mpya wa Marekani Joe Biden ameanza kutengua sera kadhaa muhimu za Donald Trump, saa chache baada ya kuapishwa. Severine Kapinga ni Mchambuzi wa maswala ya Kimataifa na Diplomasia amejaribu kuzungumzia mambo mbalimbali yatakayo mkabili Rais Biden na kile kilichomuangusha Donald Trump katika uchaguzi uliyopita. Yote hayo utayapa kwa kina ukiingia YouTube kisha na kuandika Bongofive

IMEANDIKWA NA Hamza Fumo Instagram natumia @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents