Burudani

Uchambuzi: Kwanini Born Sinner ya J-Cole ni kali kuliko Yeezus ya Kanye West, albam zote zimeachiwa leo

Kanye West (Yeezus) na J. Cole (Born Sinner) wote wameachia albam zao leo na hiyo ina maana moja tu: Ushindani. Pale rappers wakubwa wanapoachia albam zao siku moja ni kitu kizuri kwenye kiwanda cha muziki.

page

Ni ushindani mkubwa kati ya J-Cole na Kanye West ambapo Kanye ni kama kaka kimuziki kwa J-Cole. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa wote ni maproducer hivyo wamehusika kwa kiasi kikubwa katika mchakato wa utayarishaji wakishirikiana na wapishi wengine.

Maproducer walioshiriki kutengeneza albam ya Kanye ni pamoja na Daft Punk, Mike Dean, The Heatmakerz, Hudson Mohawke, No ID, Rick Rubin,Rza, Travis Scott, Symbolyc One, Kanye West na Young Chop.

Yeezus – Kanye West

large_20130518-yeezus-306x-1369078235

Niseme labda mimi ni miongoni mwa wale watu wanaopenda sana nyimbo zenye beat nzuri. Hivyo kwa upande wa Yeezus nahisi sijakipata kile nachokihitaji. Nyimbo nyingi kwenye albam hii zina beat za ajabu ajabu hivi!

Zinaweza kuwa ni beat ngumu, classic, zenye ubunifu mkubwa lakini kwangu nahisi hazijanishika kivile. Kidogo nimependa Hold My Liquor hasa kwakuwa zile distorted guitar za mwisho zinanifanya zinipeleke mbali kifikra.

Blood On The Leaves ambayo muda mfupi uliopita nimeona Swizz Beatz akisema kwenye Instagram kuwa anaisikiliza kwa kuirudiarudia, nimeipenda hasa kwakuwa ina beat inayochezeka na ina brass fulani za kuvutia zikipiga kwa sauti kubwa.

Kanye kanikuna zaidi kwenye Guilt Trip na hapo kidogo ndio nikaanza kuielewa Yeezuz. Beat ya wimbo huu ni miongoni mwa zile beat ambazo zinaweza kukuchukua hata siku nzima ukiziskiliza bila kuchoka na ina vitu vingi ndani yake. Nimependa walivyoichezea chorus kwa kushusha chini pitch ya sauti. Kwa upande wangu hii ndio ngoma kali zaidi kwenye albam hii.

Yeezuz ni classic albam, yenye uzamani fulani ambao nahisi mashabiki wa hip hop ya kizamani wanaweza kurelate nayo. Kwa wapenzi wa hip hop ya sasa sidhani kama Yeezus ni albam yao kabisa. Hata hivyo kwa uzoefu wa albam zilizopita za Kanye, hii nayo inaweza kuuza sana sokoni.

Sikiliza vipande vya nyimbo zote hapa.

Born Sinner – J.Cole

tumblr_mefhpi9BzD1re5stco1_r1_1280

Kwa upande wa J. Cole yuko vizuri sana na siku zote huwa na ujumbe wa maana kwenye muziki wake. J. Cole ni mmoja wa wasanii wa hip-hop ambao unaweza kucheza albam nzima hata mbele ya mzazi (wazazi wa Marekani) na asilalamike. Ujumbe kwenye nyimbo zake ni wa tofauti sana kuliko wasanii wengine wa mainstream.

Tofauti na albam ya Kanye ambayo amewaachia maproducer wengine waguse beat zake, J.Cole ameproduce karibu ngoma zake zote yeye mwenyewe (si jambo geni kwakuwa albam zote za mwanzo alifanya hivyo pia licha ya kuweka maproducer wengine wachache). Waliomsaidia ni pamoja na Elite, No I.D na S1.

Wimbo wa kwanza tu, Villuminati unanikuna na beat yake inayopiga kiaina yake. Wow, J kaimprove sana kwenye upande huo, amenikuna. Uzuri wa albam ya J.Cole tayari ana wimbo unaofanya vizuri sasa hivi, Power Trip aliomshirikisha Miguel na hivyo kuipa thamani ya kwanza albam yake tofauti na Kanye ambapo mpaka sasa Yeezus haina hit single sokoni.

Ukitaka track classic kwenye albam hii basi nakushauri usikilize track ya 7, Run Away. Nimependa kila kitu kwenye ngoma hii na hapo J ananidhihirishia kuwa huwezi kumweka na hawa rappers wapya kabisa (ukimtoa Kendrick Lamar).
Chaining Day nimeipenda pia hasa kwakuwa amelay low kidogo na kunikumbusha kama alivyorap kwenye In the Morning aliyomshirikisha Drake.

Amekuja kunikosha zaidi kwenye Crooked Smile aliyowashirikisha TLC. Bonge moja la ngoma na nahisi kama akiichia itafanya poa sana.

Sikiliza vipande vya nyimbo kwenye Born Sinner hapa

Kwa uchambuzi huo mfupi, kwangu mimi Born Sinner ya J.Cole ni kali zaidi kuliko Yeezus ya Kanye West. Sijui mtazamo wako ukoje,..

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents