Michezo

Uchawi wamponza Lukaku kwa bosi wa Everton

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku anakusudia kumfikisha mahakamani mmiliki wa Everton Farhad Moshiri kufuatia madai yake kuwa mchezaji huyo aliamua kuondoka baada ya kupata ushauri kutoka kwa mganga wa kienyeji uliyomtaka kufanya hivyo.

Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku 

Moshiri aliyasema hayo wakati wa kikao cha mwaka cha wamiliki wa hisa za klabu hiyo siku ya Jumanne nakudai kuwa ujumbe huo ulimtaka Lukaku kukataa kupokea ofa mpya ya kiasi cha paundi 140,000 kwa wiki ndani ya Everton na badala yake ajiunge na Chelsea ndipo ghafla akaiambia klabu kuwa anahitaji kuondoka.

Mmiliki wa klabu ya Everton, Farhad Moshiri akieleza kwanini Lukaku hakusaini mkataba mpya

Hatimaye akajiunga na Manchester United kwa dili la nono la paundi milioni 75, hivyo ndivyo Mushiri ameuambia mkutano huo wa mwaka wa AGM sababu za Lukaku kuondoka.

Lukaku anahisi kuumizwa na Moshiri, kufuatia matamshi yake aliyosema hadharani.  “Tulimpatia ofa nzuri zaidi ya ile ya Chelsea na wakala wake alikuja kwaajili ya kusaini makubaliano hayo,” amesema Moshiri .

“Na ghafla katikati ya mazungumzo akasema ameitwa na mama yake ambaye yupo Afrika  na ndipo alipopata ujumbe huo wa mganga wa kienyeji uliyomtaka aende  Chelsea,”.

“Lukakukilasiku alikuwa akitamani kuondoka Goodison Park na wala halikuwa swala la kifedha,” amesema Moshiri ambaye kwa sasa mchezaji huyo anaangalia ni kwa namna gani anaweza kumfikisha mahakamani.

Mshauri wa Lukaku amesema kuwa maneno yaliyozungumzwa na Moshiri yamemuaribia taswira ya mchezaji huyo, kwakuwa maamuzi ya Lukaku kuondoka Everton hayahusiani na maswala ya imani za kishirikina  bali yalikuwa ni maamuzi binafsi.

“Sasa ataona hatua zitakazochukuliwa na mahakama na namna mahusiano yao yatavyokuwa, Romelu ni mkatoliki safi na uchawi siyosehemu ya maisha yake na wala hanaimani na maswala hayo,” amesema mshauri huyo.

“Ukweli nikwamba hakuwa na imani na mipango ya Mr Moshiri juu ya Everton, ndiyo maana akakataa kusaini mkataba mpya na kuhitaji kupiga hatua nyingine katika tasnia yake ya soka.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents