Habari

Uchunguzi: Wanajeshi wa Australia walitenda uhalifu wa kivita Afghanistan

Uchunguzi juu ya uhalifu wa kivita uliofanywa na wanajeshi wa Australia nchini Afghanistan umegunduwa kwamba kwa uchache raia na wafungwa 39 waliuawa kinyume na sheria, kwa mujibu wa mkuu wa majeshi wa Australia.

Australien | General Angus Campbell, Chef der australischen Verteidigungsstreitkräfte (ADF)

Akiwasilisha muhtasari wa ripoti ya uchunguzi wa miaka minne mbele ya waandishi wa habari mjini Canberra siku ya Alkhamis (Novemba 19), Mkuu wa Jeshi la Australia Angus Campbell alisema kikosi maalum cha jeshi la Australia kilihusika na mauaji hayo dhidi ya wafungwa, wakulima na raia wa kawaida.

Jenerali Campbell alisema kuna rikodi za kutia aibu kama vile mwanajeshi kumuuwa mfungwa ili tu kupata ladha ya kumuuwa mtu wa kwanza, tendo ambalo kijeshi huitwa “kumwaga damu”, na kisha baada ya mauaji kama hayo, wanajeshi walikuwa wakipandikiza silaha na redio ili kutunga madai ya uongo kwamba wahanga wao walikuwa maadui waliouawa kwenye mapambano.

Hata hivyio, kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, mkuu huyo wa majeshi alisema kilichotendwa na wanajeshi hao wachache, hakiwakilishi maadili ya walio wengi kwenye jeshi la Australia.

“Alichogunduwa Inspekta Mkuu kinakinzana kabisa na juhudi nzuri na kinaathiri mamlaka yetu ya kimaadili kama jeshi. Ripoti yake inaeleza kwa udani taarifa zinazohusiana na tuhuma zinazoumiza sana za mauaji ya kinyume cha sheria yaliyofanywa na baadhi yetu. Kwa heshima zote nawaomba watu wa Australia kuwakumbuka na kuwaamini wengi waliosalia. Nami naamini hivyo.”

Campbell alisema mauaji hayo haramu yalianza mwaka 2009, ingawa mengi yao yalifanyika mwaka 2012 na 2013.

Hakukuwa na sababu za mauaji

Australische Einheiten in Süd-AfghanistanBaadhi ya wanajeshi wa Australia nchini Afghanistan.

Mkuu huyo wa majeshi aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakuna kifo hata kimoja kati ya hivyo kilichotokea kwenye mazingira ya kivita wala katika hali ambapo wauaji walikuwa wamekabiliwa na kitisho cha maisha yao ama kuchanganyikiwa kiakili.

Akiomba radhi kwa serikali na watu wa Afghanistan, Campbell alisema washukiwa wote walioulizwa walikuwa wakifahamu vyema sheria ya vita na kanuni za kukabiliana na wengine kwenye mapambano.

“Kwa watu wa Afghanistan, kwa niaba ya Jeshi la Ulinzi la Australia, kwa unyenyekevu wote naomba radhi kwa kila ovu lililotendwa na wanajeshi wa Australia. Nimezungumza moja kwa moja na mkuu wa majeshi wa Afghanistan, Jenerali Yasin Zia, kumpa ujumbe huu. Matendo haya maovu yameikosea heshima imani ambayo watu wa Afghanistan walitupa walipotuomba kwenda kuwasaidia nchini mwao.”

Tangu mwaka 2016, kumekuwa kukifanyika uchunguzi juu ya shutuma za uhalifu wa kivita uliofanywa na vikosi vya Australia nchini Afghanistan kati ya mwaka 2005 na 2016.

Ripoti kamili ya uchunguzi huo, ambayo ilitarajiwa kuchapishwa Alkhamis, inapendekeza maafisa 19 wa kijeshi kufunguliwa uchunguzi rasmi kwa ajili ya mashitaka ya uhalifu huo wa kivita.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents