UDSM yatoa taarifa kuhusu ajali iliyoua wanafunzi, wakanusha hili

Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kupitia Wizara ya Afya na Kafteria imesema imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya ajali mbaya iliyotokea siku ya 11 June, 2018 majira ya saa tatu usiku maeneo ya Riverside

Ajali hiyo imehusisha Ambulance ya Chuo iliyokuwa na watu wafuatao
1.Soko, Maria Godian(student)
2. Steven E Sango (student)
3. Abishai Nkiko (student)
4.James (driver)

Hadi sasa wanafunzi wawili ambao ni Soko, Maria Godian (first year Coss) na Steven E Sango (CPE CoET second year) pamoja na James (dereva) wamefariki dunia.

Mwanafunzi mwingine Abishai Nkiko (Bsc Industrial Engineering third year CoET) hali yake ni mbaya na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tuendelee kumuombea apate kupona haraka.

Katika hatua nyingine Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Hussein Amri Aman, amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu mwanafunzi Maria Godian Soko aliyefariki dunia kwa ajali kuwa alikuwa mjamzito na kwamba zinapaswa kupuuzwa.

Amri ameiambia EATV, kwamba marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu na ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe anakimbizwa hospitali kwa ambulance.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW